PAUL
MAKONDA AMEWAWEZESHA WANYONGE KUTIBIWA BURE

Mkuu wa Mkoa wa Dar e s Salaam Paul Makonda amekuwa akifanya
jitihada kubwa za kuwapunguzia gharama za matibabu wananchi wenye kipato cha
kawaida(wanyonge) Ni hivi karibuni wagonjwa wasiopungua 10,000 waliweza kupata
matibabu bure. Meli iliyokuwa na madaktari bingwa kutoka nchini China ilitoa
huduma hiyo kwenye bandari ya Dar es Salaam. Wananchi wengi waliojitokeza
waliweza kupimwa na kutibiwa magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni kama vile
shinikizo la damu,Kisukari,Saratani na
mengine ambayo wananchi wa kawaida wasingeweza kutibiwa kwana gharama za
matibabu ni kubwa.
Lakini hata kabla ya madaktari hao wa kichina kuja kutoa
huduma za matibabu, mkuu huyo wa mkoa alikuwa tayari amefanya ushawishi kwa
madaktari hapa nchini kuwapima na kuwatibu wagonjwa. Watu wengi wamekuwa
wakijitokeza kupokea huduma hiyo, ingawaje idadi ya wahitaji bado ni kubwa.
Kiongozi huyo amekuwa akiwahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kupima afya
zao, kwani ni muhimu kwao kufahamu hali za afya zao ili kuweza kukabiliana na
magonjwa ya hatari.
Makonda anaamini kuwa ikiwa kila mwananchi atakuwa na afya
njema, ni dhahiri atakuwa na uwezo wa kutoa mchango mkubwa katika ujenzi wa
taifa lake. Kitu kingine ambacho Makonda ameweza kuwathibitishia wananchi
katika ubunifu huo, ni uwezo wake wa kuonesha serikali inaweza kuwatibu bila
kulipia fedha.
Enzi ya watanzania kutibiwa bure ilikoma wakati wa utawala
wa awamu ya kwanza ya hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kujitokeza kwa wingi kwa wananchi wanaohitaji matibabu ya bure, ni kiashiria
kwa serikali kutambua kwamba wananchi wanapenda kupimwa afya na kutibiwa,
lakini gharama ziko juu.
Ubunifu wa Makonda wa kupima na kutoa matibabu bure kwa
wananchi, umekuwa ukiwalenga zaidi wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam. Hata hivyo
wahitaji, wahitaji ni wengi na wakazi wa mikoa mingine wamekuwa wakijitokeza.
Kwa siku zilizopita, Rais wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli alimsifu Makonda
kwa ubunifu ambao amekuwa akiufanya na kuijengea heshima serikali yake. Alitoa
mwito kwa wakuu wa mikoa mingine hapa Tanzania kuiga kile kilichokuwa
kikifanywa na kiongozi huyo. Na ndiyo maana
basi kwamba kama wakuu wengine wa mikoa wangewahamasisha madaktari
kwenye mikoa yao, watu wengi zaidi wangenufaika na vipimo na matibabu ya bure.
Makonda alipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni aliwahamasisha
wamiliki wa magari ya abiria jijini Dar es Salaam (Daladala) kuwasafirisha
waalimu wote bure wakati wanapokwenda na kurudi kutoka kazini. Alifanya hivyo
kwa kutambua hali ngumu ya maisha inayowakabili waalimu wa mkoa wa Dar es
Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Makonda hali kadhalika anaendelea na jitihada za kuhamasisha
watu mbalimbali wasaidie mradi wa kujenga ofisi za walimu. Amepata mwitikio
ndani na nje ya nchi. Ubalozi wa China hapa nchini umetoa fedha nyingi za
kumuunga mkono Makonda ili afanikishe ujenzi wa ofisi za walimu mkoani Dar es
Salaam.
Ubunifu wa Makonda unajitofautisha na wakuu wa mikoa
wenzake. Badala ya kuamrisha taasisi,mashirika ama wananchi wafanye nini, yeye
ubunifu wake umekuwa ukilenga kuhamashisha na kisha kutanzua tatizo analoliona
kwa jamii. Kwa mfano, wananchi waliobahatika kupimwa na kutibiwa bure
watamkumbuka Makonda kuwa kiongozi anayetetea ustawi wa maisha yao kwa
kuyapigania. Wakiisha kuwa na afya njema,nao watakuwa tayari kulitumika taifa
kwa moyo wote na kuliwezesha kupata nguvu ya kiuchumi katikati ya mataifa
mengine duniani. Makonda anastahili kupongezwa kwa kutetea afya za watanzania
ambao kwao ni mtaji mkubwa.