Ntami Habari
Wednesday, May 23, 2018
RASILIMALI ZA MAJI KAMA VILE SAMAKI NI MUHIMU WALINDWE
Nchini Tanzania kumekuwa na uvuvi haramu wa Samaki. Uvuvi huo haramu umekuwa ukifanyika kwa kutumia nyavu zisizofaa, kutumia mabomu na hata kutumia sumu. Hali hiyo imekuwa ikisababisha madhara kwa samaki wachanga na hatimaye viumbe hao kupungua kwa kasi.
Katika kuhakikisha viumbe hao wanalindwa, serikali iliamua kuanzisha operesheni maalum kwa ajili ya kudhibiti uvuvi haramu. Lakini hata kabla ya kuanzishwa kwa operesheni hiyo, tayari serikali ilikuwa imetoa elimu kwa wavuvi wote ili wajiepushe na uvuvi haramu.
Kwa kuwa operesheni hiyo imefanyika nchi nzima, nyavu za wavuvi ambazo haziruhusiwi katika uvuvi huo zilichomwa moto ama kuteketezwa kabisa. Kwa kiasi kikubwa idadi ya wavuvi ambao walikuwa wakijihusisha na uvuvi haramu, mali zao zimeharibiwa.
Katika kikao cha Bunge la Bajeti linaloendelea huko mkoani Dodoma, wabunge wameonesha kutoridhishwa na jinsi operesheni hiyo ilivyofanyika. Wamelalamika kwamba wavuvi wamenyanyaswa na maofisa wa serikali waliokuwa wakisimamia zoezi hilo.
Kutokana na kutoridhishwa na mwenendo huo, wabunge hao walitoa mapendekezo ya kutaka iundwe tume ya kuchunguza ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji wa operesheni hiyo.
Kwa ujumla wake, wabunge hao walikuwa na haki yao ya kikatiba kukosoa utaratibu huo. Hata hivyo ulinzi wa rasilimali za majini ni muhimu sana kwani kwa muda mrefu uvuvi huo haramu umekuwa ukifanyika. Ni wakati kwa wavuvi wakubali kufuata maelekezo ya serikali. Walipewa muda wa kutosha waache. Walaji wa Samaki wanataka walishwe samaki wanaofaa kwa afya zao
Saturday, January 20, 2018
CHADEMA MSIPATE KIGUGUMIZI KUKUBALI KUKUA KWA UCHUMI
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimempinga mwanachama mwenzake, Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa aliyeisifia serikali ya awamu ya tano kwa kuwaletea maendeleo wananchi wake. Edward Lowassa alikwenda Ikulu na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufulil
Kwa mfano, Lowassa alisifia ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza na Kigoma. Vile vile mradi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi mkoani Tanga. Lowassa aliitaja miradi hiyo kuwa itapanua wigo wa ajira hapa nchini na kuongeza kipato.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anasema alichokizungumza Lowassa huko Ikulu siyo kauli ya chama chao. Licha ya kutokuwa kauli ya chama chao, Mbowe alimshangaa Lowassa kwa kutolizungumzia suala la kushambuliwa kwa kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu. Baadaye mbunge huyo alipelekwa kwenye hospitali ya Nairobi nchini Kenya.Kwa sasa amehamishiwa nchini Ubelgiji kuendelea na matibabu.
Mbowe vile vile anasema watanzania wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, iweje Lowassa asifie serikali kwamba hali ya uchumi ni nzuri ama inaridhisha? Naye Lissu anapinga akisema Lowassa hakupata kibali cha chama chao ili aweze kwenda Ikulu na kuzungumza na Magufuli.Mbunge wa Arusha, Godbless Lema hakubaki nyuma kumlaumu Lowassa kwenda Ikulu kumsifia Magufuli
Ni ukweli usiopingika kile kilichozungumzwa na Lowassa kwa Magufuli hakikuwafurahisha viongozi wa CHADEMA. Lakini Edward Lowassa ambaye amewahi kuwa kada wa chama cha Mapinduzi na kiongozi wa ngazi ya juu serikalini, alikuwa na haki ya kupangilia kipi cha kuzungumza anapokutana na kiongozi wa nchi.
Isingekuwa ni busara kwa Lowassa kuzungumzia suala la kushambuliwa kwa Lissu kwa Magufuli Lowassa anafahamu kuwa tayari serikali ilikuwa imelitolea ufafanuzi wa kuendelea na uchunguzi na upelelezi ili kuwanasa waliohusika. Hata kama angethubutu kulihoji angejulishwa alipeleke kwa mkuu wa jeshi la polisi kwani kwa wakati huo haikuwa mahali pake.
Kwa hali hiyo basi, kama angethubutu kulihoji ama kuliulizia lingemfedhehesa na lingeharibu ladha ama mantiki ya kwenda Ikulu.Hoja hiyo ingemsababishia Lowassa atambulike kama ni kiziwi ama jeuri kwani haikuwa nafasi ya kurudiarudia maneno yaleyale.
Ama kwa awamu hiyo ya kwanza hakuyazungumzia, yanaweza kuzungumzwa kwa awamu ijayo kwani uwezekano wa Lowassa kurudi Ikulu bado atakuwa anakaribishwa tena.Lowassa kama mwanasiasa ndiyo kwanza amefungua ukurasa mpya wa kukutana tena na kubadilishana mawazo na Magufuli.
Ni kweli Lowassa aliwachukiza viongozi wa CHADEMA eti kwa kusifia na kupongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha uchumi. Sasa viongozi wa CHADEMA walitegemea akanushe ama apuuze taarifa za wataalalmu wa uchumi kwamba uchumi unakua? Walitaka awasilishe porojo kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli? Na kwa ujasiri na umakini wa Dk. Magufuli,angekubali? Isingewezekana
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aliyestaafu hivi karibuni Profesa Beno Ndulu.amewathibitishia watanzania kwamba uchumi wa nchi unakua. Gavana huyo kwenye taarifa yake alitoa vigezo mbalimbali vinavyothibitisha kukua kwa uchumi.Mojawapo ya vigezo hivyo ni vya huduma za fedha ambavyo vimekua na kuongezeka.
Hata kabla ya kutolewa kwa taarifa ya Gavana Ndulu, Rais Dk.Magufuli alikuwa akiwaeleza watanzania kwamba uchumi wa Tanzania unakua. Amekuwa akibezwa na wapinzani kumfanya kiongozi wa nchi aonekane mwongo.
Uthibitisho wa Gavana Ndulu, unaungwa mkono na msemaji wa serikali Dk. Abbas ambaye naye anaitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano za Afrik ambazo uchumi wake unakua na kusitawi. Hivyo basi malalamiko ya viongozi wa CHADEMA yaliyomtaka Lowassa azungumze tofauti na taarifa za wataalamu, yanawatambulisha waonekane kuwa viongozi wasiopenda kusema ukweli hata pale ambapo umethibitishwa.
Na kwa kuwa viongozi hao wa CHADEMA hawataki kuukubali ukweli huo, wanawekwa kwenye kundi la maadui wa usitawi wa uchumi wa Tanzania. Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Magufuli alipokuwa akimuapisha Naibu Waziri wa Madini Doto Mashaka Biteko.
Magufuli anasema kwa wakati huu tuko mapambano makubwa na vita vya kiuchumi. Siyo kila mtu ama taifa litakuwa linafurahishwa na mapambano hayo. Lakini sasa tumeanza kuwasikia maadui wa vita hivyo hapa hapa nchini,hususani unapopatikana ushindi.
Kwamba siyo ajabu wakati watanzania tukijivunia ama kujipongeza kwa mafanikioa hayo, kundi jingine la watanzania wenzetu linaichafua ili watanzania wasipata nafasi ya kujipongeza kwamba wanafanya vizuri kiuchumi.
Kukua kwa uchumi hapa nchini kunaashiria mwitiko wa wananchi kufanya kazi kwa bidii ya kulijenga taifa lao. Lakini vile vile kukua kwa uchumi kunatokana na usimamizi wa kudhibiti ubadhirifu wa rasilimali za umma, rushwa na ufisadi. Imani ya wananchi kwa serikali yao kwamba inawatumikia na kujali maslahi ya umma, vinawapa faraja ya kushirikiana serikali yao.
Kwa upande mwingine ni ujasiri na moyo wa kizalendo unaooneshwa kwa vitendo na Rais Dk. Magufuli. Amekuwa mstari wa mbele kukataa kutafuta kujineemesha ama kujitajirisha yeye binafsi. Ameweza kutoa uthibitisho h uo katika kusimamia rasilimali za madini kwa kuzibana kampuni kulipa kodi.Ameweza kuonesha ujasiri huo akiwatetea watanzania ambao wamenyonywa kwa muda mrefu na kuwasababishia kuwa maskini.
Kwa kuwa wenzetu hawako pamoja nasi katika kujipongeza kwa usitawi wetu wa uchumi, hatutawashangaa tukiwasikia wakiwashawishi watu wafanye hujuma dhidi ya ustawi wa uchumi huo.Watafanya hivyo kwa kuwachanganya kwa taarifa zao kama wanavyofanya sasa. Inakuwaje uelewa wao unakuwa mdogo wanapopewa taarifa ambazo ziko wazi kwa manufaa ya watanzania?
Hivi hao wanaozikataa taarifa hizo za kukua kwa uchumi wa Tanzania, wanataka wao ndiyo wawe watoaji wa taarifa za hali ya uchumi wa taifa hili? Hilo kamwe haliwezekani.Wao ni vyema waendelee na siasa ambako wanaweza kufanya ubabaishaji, lakini siyo kwenye utaalamu kwenye hali ya kiuchumi.
Ama kama wanata wajipe madaraka hayo, basi ni vyema wakawafanyia wanachama wao ambao wataendelea kubaki nyuma kwa kupewa taarifa ambazo hazioneshi mabadiliko. Watanzania wapenda maendeleo wanayo shauku ya mabadiliko.Hawazipendi taarifa za kushindwa. Ni wakati wao kutembea kifua mbele kujipongeza kwa kukua kwa uchumi wao.

JE,EUTHANASIA NI MAUAJI?
Je, unadhani binadamu anapougua kwa muda mrefu anayo haki ya kuomba aharakishiwe kufa mapema?Maisha ya binadamu ni zawadi kutoka kwa mwenyezi Mungu. Hakuna uhalali kwa mtu yeyote kukatisha uhai wa mtu. Lakini baadhi ya nchi zimetoa ruhusa kwa mgonjwa aliyeugua kwa muda mrefu, kutoa idhini kwa madaktari wanaomuuguza mgonjwa kuruhusu afe mapema.Ruhusa hiyo inatia simanzi na majonzi kwa mgonjwa anapotoa ruhusa hiyo.
Uthubutu wa kuruhusu mgonjwa(mtu) ajifie mapema au haraka inatajwa kwa neno la kiingereza liitwalo'euthanasia'. Tafsiri yake inatajwa ikimaanisha kuwa ni kitendo cha kukatisha maisha ya mgonjwa ambaye inaelekea hawezi kupona, ama ni mzee.
Euthanasia inaweza kufanywa kwa aina mbalimbali. Kwa hatua ya kwanza,mgonjwa anaweza kuridhia ajifie mapema. Aina nyingine inaweza kufanyika pasipo kumhusisha mgonjwa aliye mahututi.Kwa vyovyote iwavyo,uthubutu wa kukatisha maisha ya mtu ambaye ni mgonjwa, haukubaliki kwani ni wa kujichukulia madaraka ya mwenyezi Mungu ambavyo sivyo.
Katika imani ya kikristo,mgonjwa anapokuwa mahututi huombewa kwa mwenyezi Mungu ili mapenzi yake amuepushe na kifo.Lau kama siyo hivyo basi kama akimchukua, ampokee katika ufalme wake.
Nchini Tanzania kumekuwa na matukio ya watu kujinyonga. Baadhi wamekuwa wakifanya hivyo kutokana na wivu wa kimapenzi, kushindwa mitihani, madeni sugu na mengineyo mengi. Maamuzi hayo yamekuwa yakichukuliwa kama suluhisho la kilichowakuta. Vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu, vinakataza wanadamu kuchukua maamuzi ya kukatisha maisha yao. Vinawaelekeza kazi hiyo wamuchie mwenyezi Mungu pekee. Mathalani kwenye Biblia kitendo hicho kinatajwa kuwa ni dhambi.
Kwenye biblia hiyohiyo, inasema kwa kuifanya dhambi hiyo kutakuwa na swali la kujibu kwaa nini binadamu alichukua uamuzi huo
Kwa sheria za Tanzania, ni kosa kwa mtu kukatisha maisha yake. Ndiyo maana endapo mtu aliyekusudia kukatisha maisha yake akishindwa kufanikisha lengo hilo, anashitakiwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria
Katika utamaduni wa kiafrika inatambulika kuwa kifo ni lazima. Lakini katika hali ya kawaida kulazimisha kufa ni uamuzi unaowashitua wengi. Kifo kipo na kinapotokea kwenye familia kinasababisha ;pengo Kuna watu waliokuwa wakimtegemea marehemu, ambao baadaye huathirika.
Matukio ya watu kukatisha maisha kwa kujinyonga, kunywa sumu ama mengineyo yamekuwaa yakitajwa kuwa yanaweza kupata suluhu. Wanasaikolojia wanasema ushauri nasaha ni muhimu kwa watu wanaoonesha kukata tamaa ama dhamira ya kukatisha maisha yao mapema. Lakini vile vile kuwa na subira ni muhimu ili kuepukana na janga hilo

Subscribe to:
Posts (Atom)